Benki ya Exim kuinunua rasmi Benki ya UBTL

|
Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu

Ikiwa na lengo la kutanua mizizi yake kibiashara nchini, Benki ya Exim Tanzania imeonyesha nia ya kuinunua rasmi Benki ya United Tanzania Limited (UBTL) kwa asilimia 100. Hii ni baada ya kutiliana saini barua ya kuonesha nia hiyo (Letter of Intent).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu, ununuzi huo unahusisha mali na madeni unaozidi kuifanya benki hiyo ambayo kwa sasa ni miongoni mwa benki tano kwa ukubwa nchini kuzidi kujitanua zaidi ndani na nje ya nchi.

“Kwetu ni furaha kubwa kuona kwamba familia yetu inazidi kuongezeka kwa kuwa tayari tunaungana na wanafamilia kutoka Benki ya UBTL. Zaidi ya yote tunaamini pia kuwa wafanyakazi wa benki hiyo wataongeza nguvu ambayo kwa pamoja tutaweza kutoa huduma bora zaidi za kibenki kwa wateja wa UBTL,’’ alisema Matundu.

Fedha
Maoni