BoT yazionya benki zinazochelewa malipo ya Korosho

|
Bidhaa ya Korosho ikisubiri kuchukuliwa sokoni

Benki Kuu Tawi la Mtwara imezionya benki zitakazoendelea kuchelewesha malipo ya wakulima wa korosho na vyama vya msingi vya mikoa ya kusini  na kuongeza kuwa atakayebainika kuendelea kufanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa.

Hatua hiyo imekuja kufuatia malalamiko yaliyotolewa na wakulima na vyama hivyo vya msingi wakidai kucheleweshewa fedha zao wakati wa mauzo, kupitia utaratibu uliowekwa na serikali kuwa malipo yote yafanywe kupitia benki.

BoT Mtwara wameingilia suala hilo ikiwa imesalia miezi michache kuelekea msimu wa mauzo ya zao la korosho na kuzitaka benki hizo kuachana na tabia ya kuendesha shughuli zake kwa matakwa yasiyozingatia sheria.

Kwa mujibu wa Mwanasheria wa Benki kuu hiyo mkoani Mtwara, Ramadhan Miyonga imewataka wale wenye malalamiko kukitumia vyema kitengo cha dawati la migogoro na kuweza kupatiwa ufumbuzi wake kwa wakati.

Msimu wa mwaka 2017-2018 kumekuwepo na tatizo la baadhi ya wakulima wa zao la kororsho kucheleweshewa kulipwa fedha zao kwa zaidi ya wiki moja hadi tatu na hasa pale vyama vya msingi vilipotakiwa kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda izwa bank nyingine.

Kilimo
Maoni