Brexit kujitoa EU, ajira 500,000 za Waingereza mashakani

|
Baadhi ya waandamanaji wakishinikiza Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya

Meya wa jijini London, Sadiq Khan amesema nafasi laki tano za ajira huenda zikawa hatarini iwapo Brexit itafanyika "bila makubaliano" muafaka.

Meya huyo alitoa taarifa hiyo jana,Ijumaa mjini London ambapo alisema, takribani nafasi laki tano za ajira nchini Uingereza zitakuwa hatarini kama Uingereza itajitoa moja kwa moja kutoka Umoja wa Ulaya bila kufikia makubaliano yoyote na umoja huo.

Ripoti hiyo imesema Brexit iwapo itajitoa bila makubaliano yoyote ya namna ya kulinda maslahi ya wananchi wake, itakwamisha ukuaji wa uchumi wa Uingereza kwa muongo mmoja au zaidi,huku nafasi za ajira zinakadiriwa kupungua kwa laki tano, na uwekezaji ukitarajiwa kushuka kwa dola bilioni 68 za Kimarekani ifikapo mwaka 2030.

Utawala
Maoni