China walipa kisasi cha ongezeko la ushuru kwa bidhaa za Marekani

|
Vita ya kibiashara kati ya Marekani na China

Kamati ya Kanuni za Ushuru ya Baraza la Serikali la China imeamua kutoza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa za Marekani zenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 16 kuanzia  Agosti 23. 

Kamati hiyo imesema hatua hiyo inalenga kulinda kadri iwezekanavyo maslahi ya wateja na mashirika ya China.

Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China, Gao Feng amesema, uamuzi wa Marekani wa kutoza ushuru wa asilimia 25 dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 16, kwa mara nyingine tena umeweka sheria yake ya ndani juu ya sheria ya kimataifa, kitendo ambacho hakina maana.

Amesema China imelazimika kujibu hatua hiyo ili kulinda maslahi halali ya nchi na mfumo wa biashara wa pande nyingi duniani.

Biashara
Maoni