Dkt. Ashatu awahimiza wana Kondoa kuchangamkia fursa mkoani Dodoma

|
Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu waziri wa Mipango na Fedha

Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amewata wakazi wa Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma kuchangamkia fursa za mkoani Dodoma kuwa makao makuu ya nchi kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali za kilimo kwa kuwa mji wa Dodoma sasa ni soko la uhakika.

Dkt. Kijaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ametoa rai hiyo alipotembelea Kata ya HAUBI wilayani humo kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo katika sekta za afya na elimu.

Amesema kuwa serikali imejitahidi kuboresha miundombinu ya barabara pamoja na maji na kuwataka wakazi wa Wilaya ya Kondoa kujishughulisha na kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia maji ya visima virefu vilivyochimbwa na vinavyoendelea kuchimbwa wilayani humo.

Dkt. Kijaji amewataka wazazi wa wilayani humo kuwahimiza watoto wao kusoma kwa bidii ili vijana wao wa kike na wa kiume waweze kupata elimu bora itakayowawezesha kushiriki kikamilifu katika uchumi wa viwanda.

Biashara
Maoni