Dkt. Shein akubali kushirikiana na Indonesia kibiashara

|
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasili visiwani Zanzibar akitokea nchini Indonesia

Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein amesema Serikali ya Indonesia imekubali kushirikiana na Zanzibar katika nyanja mbalimbali ikiwemo Uvuvi, Biashara na Kilimo Cha Mwani.

Akizungumza mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akitokea nchini Indonesia kwenye ziara ya siku saba amesema ni vyema wananchi washirikiane kikamilifu na wawezekaji wenye nia ya kuwekeza visiwani humo.

Dkt. Shein amesema Serikali itahakikisha inaliinua zao la mwani ili wakulima waweze kunufaika na zao hilo.

Biashara
Maoni