Elimu matumizi ya dawa za kuulia wadudu yahitajika Singida

|
Zao la pamba Singida

Elimu ya matumizi bora ya dawa ya kuulia wadudu waharibifu wa pamba bado inahitajika kwa wakulima wa pamba wilayani Ikungi mkoani Singida.

Hitaji hilo limekuja baada ya dawa wanayoitumia sasa kutoua wadudu waharibifu katika baadhi ya mashamba katika Kata ya Kikio wilayani humo.

Licha ya suala hilo la elimu kuhitajika, Wizara ya Kilimo na umwagiliaji imeomba ufanyike utafiti sahihi wa dawa ipi itakayofaa kuua wadudu hao waharibifu wa pamba.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungu, Miraji Mataturu alipotembelea mashamba ya wakulima hao wa Kata ya Kikio na Msughaa.

Hata hivyo kilimo hicho cha zao la pamba kinalimwa kwa njia ya mkataba kati ya wakulima na kampuni iliyopewa dhamana ya kununua pamba hiyo mkoani Singida ya Biosustain ambapo kilo moja itanunuliwa kwa shilingi 1,100 kwa kilo.

Kilimo
Maoni