Emirates wazindua ndege yenye madirisha bandia

|
Mfano wa madirisha yatakayokuwa kwenye ndege mpya za Emirates

Kampuni ya Ndege ya Emirates imezindua ndege ambayo imetengezwa na madirisha ya bandia.

Badala ya abiria kuweza kuona nje moja kwa moja, sasa watalazimika kutazama picha kutoka nje wakiwa ndani kwa kutumia kamera za fibre-optic

Emirates inasema kuwa hatua hiyo inatoa fursa ya kuondoa madirisha yote katika ndege za siku zijazo, suala litakalozifanya kuwa nyepesi na kuongeza kasi yake.

Rais wa Emirates, Sir Tim Clark amesema kuwa picha hizo ni nzuri ikilinganishwa na picha zinazotazamwa kwa macho.

Madirisha hayo bandia yanapatikana katika chumba cha kwanza cha ndege aina ya Boeing 777-300Er .

Sir Tim aliiambia BBC, lengo lao ni kuwa na ndege isiyo na madirisha kabisa.

''Fikiria ndege isiyo na madirisha kabisa lakini unapoingia ndani kuna madirisha'', alisema.

Hata hivyo maafisa wa usalama wa angani kutoka mamlaka ya kudhibiti anga barani Ulaya  walisema: Hatuoni changamoto yoyote ambayo haiwezi kukabiliwa ili kuhakikisha kuwa kiwango cha usalama sawa sawa na kile cha ndege ambayo ina madirisha ya wahudumu wa ndege.

Profesa Braithwaite alisema kwamba kizuizi kikuu katika ndege isiyo na madirisha itakuwa abiria wanavyohisi kuhusu teknolojia hiyo.

Hata hivyo taarifa ya ujio wa ndege hiyo umekumbana na ukosoaji wa hapa na pale wa namna wahudumu wa ndege watakavyoweza kuona hatari iwapo itatokea.

Usafiri
Maoni