Fastjet yajiongeza, kuanza kutoa viburudisho bure

|
Ndege ya Fastjet

Kampuni ya Ndege ya Fastjet, leo Jumatatu imetangaza kuanza rasmi kutoa huduma ya viburudisho sanjari na kumruhusu mteja kusafiri na begi la kilo 23.

Kupitia taarifa yao kwa vyombo vya habari, Shirika hilo la Ndege la FastJet limesema huduma hizo zitaanza leo Jumatatu kwa wateja wote.

“Hii imetokana na utafiti tulioufanya kwa miezi kadhaa kwenye soko na kuangalia ni nini wateja wanahitaji kutoka kwa Fastjet, hivyo tukaona tubadili ‘Big saver na Achiever’ kwa kuweka huduma ambayo inakuwa katika kifurushi kimoja.
 
“Tumewasikiliza wateja wetu” alisema Mkurugenzi mkuuwa FastJet, Nico Bezuidenhout, ambaye amesema, baada ya kuyachambua kwa kina maoni ya wateja wao, wameamua kuboresha huduma zao kwa kuwa wanawathamini.

Ameongeza kwamba Fastjet itaendelea kuwapa wateja wote bei ambazo wanaweza kuzimudu.“Kama shirika linalowapa wateja thamani ya pesa yao tumejidhatiti katika kuhakikisha usafiri wa anga unabakia kuwa wa bei nafuu na zinazoweza kutumiwa na watu wote.

Kwa mujibu wa hivi karibuni Fastjet iliongeza safari ya pili kati ya Mbeya na Dar es Salaam, sambamba na safari kati ya Dar es Salaam hadi Harare inayokuwa kila siku za Jumatano pamoja na kuongeza safari ya nne kati ya Dar es Salaam na Mwanza.

“Baadaye mwaka huu Fastjet inatarajia kuongeza safari kwa nchi za Tanzania, Msumbuji na Afrika ya Kusini”. Bezuidenhout amesema kwamba huduma hii mpya itaanza kupatikana kwa safari zote za Fastjet kuanzia Agosti 6, 2018.

Biashara
Maoni