Harusi ya Harry na Meghan yaamsha vita ya bei

|
Bidhaa ambazo zinagombewa huku zikiwa na tofauti kubwa ya bei
Harusi ya Prince Harry na Meghan Markle imeamsha vita ya bei kati ya wachuuzi rasmi wa bidhaa za harusi hiyo dhidi ya wale wa mtaani kwa ajili ya kuelekea siku hiyo kubwa.
 
Wafanyabiashara rasmi wa bidhaa hizo ni wale wanaotengeneza vikombe vikubwa kwa kutumia malighafi ya china ambao wanauza kikombe hicho kimoja kwa pauni 55 ndani ya maeneo ya kasri la Windsor ambao sasa wanashindana na maduka ya wenyeji na wa mitaani wanaouza vifaa bidhaa mbalimbali kwa pauni 10.
 
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka kasri la Kifalme, sehemu ambayo Prince atamfanya Meghan kuwa Princess katika kanisa la St George bidhaa kama sahani na vikombe na visahani vyake vitapatikana kwa bei ya pauni 55.
Biashara
Maoni