Kiwanda cha Dangote chatangaza kuanza uzalishaji tena Mei 22

|
Kiwanda cha Saruji cha Dangote Mtwara

Uongozi wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote umewahakikishia Watanzania kuwa uzalishaji wa bidhaa hiyo utaanza rasmi tena mwezi Mei 22 kufuatia kufungwa wa kiwanda hicho kwa ajili ya kupisha ubadilisha wa mitambo kutoka ile ya kutumia makaa ya mawe kwenda gesi asilia ambapo zoezi hilo limekamilika kwa kiasi kikubwa.

Uongozi  wa kiwanda hicho umemwambia Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Gelasius Byakanwa alipotembelea kiwanda hicho kuwa, licha ya kujipanga kurejea kwenye uzalishaji kwa muda huo, huenda tatizo la ucheleweshaji na utoaji wa vifaa vya kisasa kutoka bandarini ukawa kikwazo cha kufunguliwa kwa wakati kiwanda hicho.

Akitembelea kujionea hatua za ujenzi wa kampuni ambayo inachakata  gesi asilia kuelekea kwenye Kiwanda cha Dangote, Mkuu wa Mtwara, Gelausis Byakanwa amesema ana panga kukutana na uongozi wa mamlaka hizo  ili ziweze kutoa vibali haraka kwani kusimama kwa shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho kuna sababisha pato la taifa na shughuli za ujenzi  kusimama.

Katika hatua nyingi Byakanwa ametembelea Mamlaka ya Bandari mkoani humo na kuzindua boti ya ulinzi ambapo amesema maeneo ya bahari yamekuwa na changamoto nyingi hususani kukosekana kwa boti za doria ambapo kwa ujio wa boti hiyo kuimarisha ulinzi huku Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Nelson Mnali akilalamikia wizi hususan wa betri za Minara na kusema ujio wa boti hiyo utasaidia kupambana na tatizo hilo.

Katika siku za hivi karibuni mkoani Mtwara bidhaa ya saruji imepanda maradufu kutoka bei ya shilingi 10,000 hadi kufikia shilingi 22, bei ambayo ni kubwa ikilinganishwa na kipato cha wakazi wake.

Biashara
Maoni