KQ sasa kwenda Marekani moja kwa moja

|
Ndege ya KQ kuanza safari za Marekani

Shirika la Ndege la Kenya, Kenya Airways, limeanza safari za moja kwa moja kuelekea nchini Marekani kutokea jijini Nairobi nchini humo.

Hatua hii  inalifanya shirika hilo kuwa la kwanza kutoka Afrika Mashariki kuwa na safari za moja kwa moja kuelekea nchini Marekani.

Kenya inataraji kuanza safari hizo mwezi Oktoba, mwaka huu baada ya miaka kadhaa ya kuzuiwa na Mamlaka za Marekani kutokana na sababu za kiusalama kutokana na Kenya kukabiliwa na mashambulio na vitisho kutoka kwa kundi la Al-Shabaab kutoka eneo la nchi jirani ya Somalia.

Suala la Usalama kuhusu ndege za moja kwa moja Marekani limefanyiwa kazi na serikali ya Kenya.  Lakini pia na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ya Kenya kuna kaguzi kadhaa zimefanyika na mamlaka za Marekani TSA pamoja na wengineo na wote wameonyesha kuwa safari kutoka Jomo Kenyatta kwenda Marekani inawezekana.

Katika taarifa hiyo bado kuna baadhi ya vitu vinaonekana kuendelea kufanywa lakini tumeamua kuwa kulingana na taarifa tulizonazo kutoka viwanja vya ndege tunaweza kuandaa na kuanza shughuli mwishoni mwa mwaka huu,

Safari hiyo itachukua saa 15 kutoka New York hadi Nairobi na saa 14 kutoka Nairobi hadi New York kwa kutumia tani 85 za mafuta huku Kenya Airways ikipanga kutumia ndege zake za kisasa aina ya Boeing 787 Dreamliner ambazo hubeba abiria 23.

Kenya Airways itafanikisha safari hizo kwa ushirikiano na Shirika la Delta Airlines la Marekani ambapo safari ya kwanza inatarajiwa kuwa Oktoba 28, mwaka huu ikitarajiwa zitawasaidia katika mpango wake wa ukuaji na kuvutia zaidi abiria na hususan watalii.

Kwa mujibu wa Bodi ya Utalii Kenya hupokea watalii 100,000 kutoka Marekani kila mwaka na kuanza kwa safari hizo kunatarajiwa kurahisisha watalii kuzuru Kenya kwa kupunguza muda wa kusafiri na gharama.

Biashara
Maoni