Kwa Mrombo kivutio kwa walaji wa nyama choma

|
Uchomaji wa nyama unaovutia wengi jijini Arusha

Ulaji wa Nyama choma kwa wenyeji wa Mkoa wa Arusha limekuwa jambo la kawaida sana pengine kutokana na asili ya wenyeji wa mkoa huo ambao ni Jamii za kifugaji hususani Wamaasai, Wameru pamoja na mwingiliano wa makabila mengine wakiwemo wachaga.

Katika viunga vya Mkoa wa Arusha lipo eneo mahsusi kwa ajili ya uchomaji na ulaji wa nyama ya mbuzi pekee likijulikana kama KWA MROMBO huku nyama inayoandaliwa hapo ikitajwa kuwa na ladha ya pekee.

Japokuwa si eneo lenye umaridadi kwa maana ya mazingira ya kuvutia lakini cha kustaajabisha ni kwamba watu wengi wanaoingia jijini Arusha kwa shughuli mbalimbali ikiwemo biashara na mikutano wamekuwa wakifurika eneo hilo kwa ajili ya kujilia nyama ya mbuzi na kondoo.

Biashara
Maoni