Malori 14 ya ufuta yazuiwa Lindi

|
Baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wakisafirisha ufuta wao baada ya kukamatwa

Maroli 14 yanashikiliwa mkoani Lindi kwa tuhuma za kusafirishwa kinyume cha utaratibu zaidi ya Kilogramu 500,000 za Ufuta sawa na zaidi ya Tani 530 huku baadhi ya Wafanyabiashara waliokuwa wakisafirisha bidhaa hiyo wakilalamika kuwa wamekamatwa kimakosa kwa kuwa wamefuata taratibu.

Wakati wakitoa malalamiko hayo, Kikosi kazi cha Wilaya ya Kilwa kimesema makosa yaliyofanywa na wafanyabiashara hao ni pamoja na baadhi ya magari kutokuwa na Hati ya kusafirishia, kutogongwa mihuri ya Chama cha msingi ilipotoka mizigo na baadhi yakibeba mizigo yenye Hati za kusafirishia zilizokwishatumika.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ilifika kwenye eneo ambalo magari hayo yamezuiwa katika kizuizi cha Marendego na Mkuu wa Wilaya, Christopher Ngubiagai amesema  suala hilo litashughulikiwa na kwamba wafanyabiashara hao wanachotakiwa ni kufuata taratibu zinazotakiwa.

Biashara
Maoni