Mchakato wa kulipa wateja wa benki zilizofilisiwa kuanza

|
Mkurugenzi wa Bodi ya Bima ya Amana, Emmanuel Boaz akizungumza na waandishi wa habari

Bodi ya Bima ya Amana iliyokabidhiwa kazi ya Ufilisi wa Benki tano zilizofutiwa leseni ya uendeshaji imeanza mchakato wa makabidhiano ili hatimaye malipo yaanze kufanyika kwa wateja huku wale wenye madeni makubwa wakItakiwa kusubiri mchakato wa ufilisi kabla hajaanza kulipwa.

Mkurugenzi wa Bodi ya Bima ya Amana, Emmanuel Boaz amesema wanatambua kuna wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu walioathirika kutokana na fedha zao za mkopo kupitishwa kwenye Benki hizo lakini watapaswa kuvuta subira ili utaratibu ufuatwe kwa kila mteja.

Boaz amebainisha hayo kwenye mahojiano mahsusi na mwandishi wa AZAM TV, Sheila Mkumba yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Fedha
Maoni