Ndege mpya ya Airbus A220-300 yaanza safari za ndani

|
Ndege mpya aina ya Airbus A220 -300

Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limezindua safari za ndani kwa ndege mpya ya Airbus A220-300 ambayo imeruka leo, Jumatano katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere hadi katika Kiwanja cha Ndege cha Mkoa wa Mwanza ikitumia takribani saa 1:10.

Mkuu wa kitengo cha mahusiano na Mawasiliano ATCL Josephat Kagirwa amesema shirika linazidi kuimarika na wamejipanga kuhakikisha wanatumia ndege hizo kuzalisha kwa faida wakitoa huduma za uhakika na usalama kwa watanzania.

Kagirwa amesema, Ndege hiyo imeanza safari za ndani huku ikipokelewa vyema na watumiaji, na kwasasa ndege hiyo itakuwa ikiruka katika mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro na Mbeya kwa kadiri uhitaji utakapoonekana.

Amesema, Ndege hiyo ina uwezo wa kwenda kwa haraka na inauwezo wa kuchukua abiria na mizigo na kusisitiza kuwa bei za shirika hilo ni nafuu.

Biashara
Maoni