Sakata la ushuru wa chuma kati ya AU, Marekani laendelea

|
Ushuru wa chuma

Kamishna wa Kamati ya Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya biashara, Cecilia Malmstrom, amesema Umoja wa Ulaya na Marekani zitaendelea kufanya mazungumzo kuhusu ushuru wa bidhaa za chuma na alumini.

Cecilia Malmstrom amekutana na mwakilishi wa biashara wa Marekani, Robert Lighthizer ambapo wamejadili kuhusu kufuta ushuru wa bidhaa za chuma na alumini za Umoja wa Ulaya zinazouzwa nchini Marekani.

Baada ya mazungumzo hayo, Malmstrom amesema mchakato halisi wa kusamehe ushuru huo bado haujulikani lakini wataendelea na mazungumzo wiki hii.

Biashara
Maoni