Sekta ya Utalii wataka kuunganishwa nguvu za pamoja

|
Utalii Tanzania, maonesho ya utalii kuratibiwa kwa ushirikiano

Wadau wa Sekta ya Utalii nchini wamesema ipo haja ya kuunganisha nguvu ya pamoja baina ya watoa huduma za Utalii na Serikali kwa ajili ya kuandaa maonyesho ya pamoja ambayo ni njia mojawapo inayotumiwa na mataifa mbalimbali duniani ikilenga kuwavuta watalii wengi kwa wakati mmoja.

Katika Bara la Afrika maonyesho ya utalii yanayoonekana kuwa makubwa zaidi ni yale ya Indaba yanayofanyika kila mwaka nchini Afrika ya Kusini.

Katika kufikia azma hiyo kwa mara ya kwanza Tanzania itashuhudia Maonesho ya Utalii ambayo yataunganishwa kutoka yale ya Kili na Karibu Fair yaliyokuwa yakifanyika kwa namna tofauti kwenye mikoa ya Kilimanjaro na Arusha huku yakielezwa kuleta mgawanyiko usio na tija.

Waandaji wanasema kusudi la muungano huo ni kuzileta pamoja kampuni zinazotoa huduma za kitalii na watalii kutoka pande mbalimbali za dunia ili kutoa taarifa kuhusu vivutio vya Tanzania.

Utalii
Maoni