Serikali imetakiwa kusaidia vituo vya kufungashia vya bidhaa za kilimo

|
Baadhi ya vifungashio ambavyo serikali inaombwa kuanzisha vituo vyake nchini

Kamati  ya Bunge ya Kudumu ya  Kilimo, mifugo na  maji imeitaka Serikali kusaidia uwezeshaji wa vituo vya kufungashia bidhaa za kilimo ili kuongeza ajira pamoja na kudhibiti  wafanyabiashara wanaoingia nchini  kununua bidhaa  na baadaye kujimilikisha kwa kuweka nembo  zinazoonesha kuwa bidhaa hizo zinazalishwa nchini kwao.

Katika kikao hicho, Kamati ya Kilimo  imepata wasaa wa kujionea namna ufungashaji wa matunda ya parachichi unayofanyika na kuibuka kwa vikwazo vya biashara hiyo.

Miongoni mwa changamoto inayotajwa ni kukosekana kwa vituo vya kufungashia, lakini pia kuwepo kwa  baadhi wafanyabiashara wanaofika na kununua bidhaa na baadaye  kujimilikisha, hali inayopoteza uhalali wa taifa kuwa wa utambulisho wa bidhaa katika masoko ya nje.

Baadhi ya wakulima wameomba kuwepo kwa mipango  itakayosaidia uwekezaji mkubwa katika sekta ya  kilimo.

Biashara
Maoni