Shehena ya kwanza muhogo mkavu yawasili China

|
Mhogo mkavu uliowasili nchini China kama makubaliano

Shehena ya kwanza ya Muhogo mkavu kutoka Tanzania kwenda nchini China imewasili katika Bandari ya Qingdao kufuatia makubaliano kati ya nchi hizo mbili yanayofungua mlango wa bidhaa hiyo kuingia katika soko la China.

Kupitia ukurasa rasmi wa Twitter wa Ubalozi wa Tanzania nchini China, shehena ya kwanza ya Muhogo mkavu iliyowasili China ni ya Makontena manne ikiwa ni ukurasa mpya kwa zao la Muhogo kuwa miongoni mwa mazao ya biashara.

Mwezi Mei mwaka jana nchi za Tanzania na China zilitiliana saini mkataba wa kuruhusu kusafirisha muhogo mkavu.

Kupatikana kwa fursa hii ya kibiashara kunatokana na China kuazimia kupunguza matumizi ya nishati ya petroli na makaa ya mawe kufikia mwaka 2020, mbadala wa nishati hiyo ndiyo unaofungua fursa ya biashara ya Muhogo mkavu ambayo inatumika kwa matumizi mbalimbali nchini humo.

Biashara
Maoni