TABOA waomba muda zaidi kuachana na matairi yaliyopigwa marufuku

|
Matairi ya magari makubwa

Chama cha wamiliki wa malori Tanzania (TATOA) kimeiomba Serikali kuwapa muda wa miaka mitatu hadi mitano badala ya miezi Sita ili wakamilishe mchakato wa kuondoa barabarani magari yenye matairi ya Super Single yanayosababisha uhabaribifu wa barabara.

Makamu Mwenyekiti wa TATOA, Elia Lukumai ametoa ombi hilo alipozungumza na Azam TV jijini Dar es Salaam na kuweka bayana kuwa hawapingi mabadiliko hayo ya sheria kuhusu kubadilisha matairi ya magari yao ya usafirishaji ambayo utekelezaji wake umeanzia Januari Mosi lakini wanadai muda uliotolewa hautoshi.

Chama  hicho cha wamiliki wa malori Tanzania wamesema wamewekeza katika biashara yao ya usafirishaji kwa kipindi cha kwa miaka 20 hivyo Serikali  iangalie namna gani ya kuongeza muda uliotolewa ili waweze kuendana na mabadiliko hayo ya sheria.

Mabadiliko ya sheria hiyo yamo kwenye taarifa ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi ISACK KAMWELWE aliyotoa wakati wa kuweka Jiwe la Msingi la Barabara Nane za Kimara Stop Over hadi Kibaha uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Biashara
Maoni