Takwimu: Mfumuko wa bei wazidi kushuka nchini

|
Vyakula vinavyodaiwa kusababisha kuendelea kushusha bei

Mfumuko wa bei nchini umeshuka hadi kufikia asilimia 3.3 kwa mwezi Julai ikiwa ni upungufu wa asilimia 0.1 ukilinganisha na 3. 4 ilivyokuwa mwezi Juni na hii ni kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

Ofisi ya Taifa ya Takwimu inasema hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 15 mfumuko wa bei kushuka na kufikia kiwango hicho, hali  inayodaiwa kusababishwa na kupungua kwa bei za bidhaa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo amesema kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia WA mwezi Juni 2018.

Biashara
Maoni