Tanzania, Benki ya Dunia warahisisha mfumo wa mikopo ya nyumba

|
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji (katikati) akibonyeza kengele leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuorodhesha hatifungan za Kampuni ya Mikopo ya Nyumba(TMRC) yenye thamani ya Sh.bilioni 120 kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam(DSE

Katika kuhakikisha mikopo ya nyumba inaanzishwa nchini, Serikali ikishirikiana na Benki ya Dunia imeanzisha mradi wa kuwezesha kuwepo kwa mfumo wa mikopo ya nyumba.

Mradi huo uitwao mikopo ya nyumba unalega kuanzisha mifumo ya mikopo ya nyumba kutokana na kufilisika kwa Benki ya Nyumba Tanzania mwaka 1995 ambayo ilikuwa inatoa mikopo ya muda mrefu kwa wateja kwaajili ya ujenzi na ununuzi wa nyumba za makazi.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema hayo jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kuorodhesha hatifungani yenye thamani ya shilingi bilioni 120 za Kampuni ya Mikopo ya Nyumba (TMRC) katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE).

“Mradi huu una maeneo makuu matatu ambayo ni uanzishwaji wa mfumo wa mikopo ya nyumba, uanzishwaji wa mfuko wa mikopo midogo midogo ya nyumba na kuendeleza mfumo wa ujenzi wa nyumba wa gharama nafuu kwa lengo la kuwapunguzia wananchi gharama za ujenzi na kuwa na nyumba za gharama nafuu,” alisema Dkt. Kijaju.

Amefafanua ili kutekeleza malengo hayo matatu Serikali ilikopa jumla ya Dola za Marekani milioni 100 mwaka 2010 kutoka Benki ya Dunia ili kuwezesha mradi wa mikopo ya nyumba kufikia malengo.

Mwenyekiti mpya wa bodi ya Wakurugenzi wa TMRC, Theobald Sabi amesema katika kipindi cha miaka saba, TMRC imeweza kuongeza muda wa urejeshaji mikopo kwa miaka 15 hadi 25 kutoka miaka mitano (5) - 10 kwa mwaka 2010.

Sabi amesema "Idadi ya benki zinazotoa mikopo ya nyumba zimeongezeka hadi kufikia Machi 31 mwaka 2010 kulikuwa na benki tatu huku riba ya mikopo ya ujenzi ikipungua kutoka asilimia 22 na 24 hadi asilimia 16 hadi 19.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Oscar Philemon Mgaya, amesema wameongeza asilimia 1.0 kama ziada ya kiasi cha Shilingi bilioni 12.5 bilioni kilichopatikana kutoka kwenye hatifungani.

"Baada ya Benki Kuu kushusha riba, gharama nyingine ikiwemo riba kwenye mikopo zinaweza kushuka pia," Mgaya amesema.

 

Biashara
Maoni