Tanzania yashiriki Maonesho ya Utalii China

|
Maonesho ya Utalii nchini China

Maonesho ya vivutio vya utalii nchini China kwa mwaka 2018 yameanza leo jijini Beijing na kuhusisha mataifa zaidi ya 150 kutoka sehemu mbalimbali duniani huku Tanzania ikiwakilishwa na Bodi ya Utalii kwa kushirikiana na Kamisheni ya Utalii Zanzibar.

Ujumbe wa Tanzania katika maonyesho hayo unaojumuisha pia wafanyabiashara na kampuni mbalimbali za kitalii nchini, unatumia nafasi hiyo kuvitangaza vivutio vya utalii katika maonyesho hayo maarufu duniani.

Afisa Habari wa Bodi ya Utalii nchini, Irene Mville pamoja na Afisa Mipango wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Hassan Ameir Vuai, wamesema Tanzania itanufaika vilivyo kupitia maonyesho hayo kutokana na China kuwa ni soko jipya wanapopatikana watalii ambapo idadi yao inaongezeka kwa kadri uchumi wa China unavyozidi kukua.

Mwaka 2016 Wachina milioni 120 walikwenda kutalii nje ya nchi yao na kutumia Dola za Kimarekani Bilioni 1.2 ambapo katika idadi ya watalii hao waliokuja nchini kwa mwaka huo walikuwa ni  37,000 tu.

Utalii
Maoni