TRA watangaza msamaha wa rmalimbikizo kwa madeni ya nyuma

|
Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza muongozo kuhusu msamaha wa riba na adhabu kwa malimbikizo ya madeni ya nyuma ya kodi ili kutoa unafuu kwa walipa kodi wenye malimbikizo ya madeni hayo kupata fursa ya kulipa ndani ya mwaka mmoja hadi kufikia Juni 30, mwakani.

Msamaha huu umetolewa kwa mujibu wa sheria zinazosimamiwa na TRA isipokuwa ushuru wa Forodha unaosimamiwa chini ya Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004, pamoja na mapato mengine yasiyo ya kodi ambayo TRA imepewa jukumu la kisheria la kuyakusanya kama vile kodi ya majengo na Matangazo.

Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere ametoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam huku akibainisha wadeni wote kutoa taarifa sahihi la sivyo watakuwa wameenda kinyume na sheria.

Biashara
Maoni