TRA Mbeya yalalamikiwa, yadaiwa kubambikia watu kodi

|
Mvutano wa mfanyabiashara maarufu (kulia), Moses Lusekelo na Meneja wa TRA Mbeya, Charles Bajungu katika suala zima malimbikizo ya kodi

Mamlaka ya Mapato  (TRA) imelalamikiwa na mfanyabiashara wa vinywaji mbalimbali Moses Lusekelo mkazi wa Kyela mkoani Mbeya akiituhumu kumkadiria kodi ya zaidi ya shilingi milioni 80 wakati yeye anastahili kulipa shilingi milioni 21.

Mbali na makadirio hayo Lusekelo amedai kuwa maafisa wa TRA wamekuwa wakimtishia kumfungia biashara zake endapo atashindwa kulipa fedha hizo.

Mfanyabiashara huyo amesema, suala hilo hajakumbana nalo peke yake, kwani amekuwa akikutana na wafanyabiashara wengine wakilalamikia suala hilo na kwamba ni mtambuka na kumuomba Rais Magufuli na Waziri wa Fedha, Dkt. Philipo Mpango kuingilia kati na kuliangalia kwa umakini.

Kutokana na madai ya mfanyabiashara huyo ya kukadiriwa kodi kubwa ikilinganishwa na biashara yake, Meneja wa TRA Mkoa wa Mbeya, Charles Bajungu amejibu tuhuma hizo na kudai kuwa tayari alishapokea malalamiko hayo na kuyawasilisha kwa vyombo vya uchunguzi pamoja na viongozi wa juu kwaajili ya kupatiwa ufumbuzi.

Biashara
Maoni