Uongozi Kagera Sugar wapongezwa

|
Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba katika ziara yake ndani ya kiwanda cha sukari Kagera

Serikali imekipongeza Kiwanda cha Kagera Sugar kwa jitihada zake za kuongeza uzalishaji wa sukari zinazolenga kukidhi mahitaji ya Taifa kufuatia maelekezo ya kufidia pengo la uhaba wa bidhaa hiyo nchini ifikapo mwaka 2020.

Pongezi hizo zimetolewa na mawaziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na mwenzake wa Viwanda, Charles Mwijage  walipofanya ziara katika kiwanda hicho mkoani Kagera.

Waziri Dkt. Charles Tizeba na mwenzake, Charles Mwijage wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wamefanya ziara hiyo maalum kwenye kiwanda hicho ambapo baada ya kutembelea mashamba ya miwa na sehemu za uzalishaji wameelezea matumaini yao kuhusu tatizo la uhaba wa sukari linalojitokeza mara kwa mara

Hata hivyo uongozi wa kiwanda hicho umetoa dukuduku lao la muda mrefu kuhusu uingizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi unavyowarudisha nyuma ikiwemo wale wanaotumia mifuko ya Kagera Sugar kuweka sukari ya nje kinyume cha sheria.

Uongozi wa Kagera Sugar umeeleza kuwa unahitaji dola za Marekani 40,000 kutimiza malengo ya kuzalisha sukari angalau tani 135,000 kufikia mwaka 2020/2021.

Biashara
Maoni