Usanifu wa awali Uwanja wa ndege Msalato wawasilishwa

|
Mchoro unaoonesha namna uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato utakavyokuwa.

Wahandisi wa Kampuni ya Studi ya Tunisia jana, Jumamosi waliwasilisha usanifu wa awali wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato unaotarajiwa kujengwa mkoani Dodoma.

Ramani hiyo yenye muonekano wa awali wa kiwanja hicho pia uliwasilishwa mbele ya wadau na wataalam wa usafiri wa anga nchini, jijini Dar es Salaam, ambao nao waliwasilisha mapendekezo yao.

Walioshiriki kwenye mkutano huo ni pamoja na uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) pamoja na wadau wengine wa masuala ya usafiri wa anga na viwanja vya ndege uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa JNIA, jijini Dar es Salaam.

Waliwasilisha usanifu huo wa awali ni wahandisi Marrarchi Walis na Kamel Fazhani wa kampuni hiyo ya Studi ya nchini Tunisia.

Utawala
Maoni