Ushirika Igunga wapitia utaratibu wa ununuzi wa Pamba

|
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry akizungumza na baadhi wa wakulima wa Pamba Igunga

Mkutano Mkuu wa 22 wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Igembensabo umeanza wilayani Igunga huku ukihudhuriwa na wanachama wake zaidi ya 200 ambapo pamoja na mambo mengine utapitia maagizo ya Serikali kuhusu utaratibu wa ununuzi wa pamba kupitia vyama vya msingi katika msimu huu.

Akifungua mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry amewataka viongozi wa ushirika wasio waaminifu kujiondoa mapema wenyewe kabla ya Serikali kutumia nguvu kuwaondoa.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema, Serikali itaendelea kusimamia ushirika ili dhamira na malengo ya kuanzishwa kwa ushirika nchini yaweze kutimia na kuleta manufaa kwa wakulima wanyonge.

Uzalishaji wa pamba kwa mwaka huu unatarajiwa kufikia kilo milioni 400 hadi milioni 600 ambapo wakulima watanufaika na zao hilo.

Biashara
Maoni