Utafiti: Magari yasiyotumia funguo hatarini zaidi kuibwa na wadukuzi

|
Magari yasiyotumia funguo bado hayajaanza kutumiwa kwenye nchi nyingi za Afrika lakini kwa kasi ya maendeleo ya teknolojia inadhaniwa Afrika itaanza kutumia magari hayo ndani ya kipindi cha miaka kumi ijayo

Utafiti mpya umebaini kuwa mamia ya magari maarufu duniani ikiwemo aina nne kati ya tano zinazouzwa zaidi nchini Uingereza yameripotiwa kuwa katika mashaka ya kiusalama hususani kuibwa.

Magari hayo ambayo hayatumii funguo na badala yake hutumia kitufe maalum cha kuwashia gari na kuzimia ambavyo kwa pamoja na kufunga na kufungua milango ya gari hutumia teknolojia maalum yametajwa kuwindwa zaidi na wataalamu wa mambo ya teknolojia maarufu kama “wadukuzi”.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na chama cha watumiaji magari cha Which? Umesema kwa mujibu wa taarifa za chama cha kutoa msaada wa magari barabarani cha General German Automobile Club (ADAC) magari ya Ford Fiesta, Volkswagen Golf, Nissan Qashqai na Ford Focus yako kwenye hatari kubwa zaidi.

Wezi wanatajwa kutumia teknolojia za juu zaidi kuweka kuvuka kikwazo cha usalama wa magari hayo hivyo kuongeza uwezekano wa magari hayo kuwa katika hatari ya kuibwa.

Hata hivyo utafiti huo umepingwa na chama cha watengeneza magari na wauzaji cha Society of Motor Manufacturers & Traders (SMMT) kilichosema "magari mapya yako salama zaidi kuliko wakati wowote ule".

ADAC imesema imeyafanyia majaribio magari 237 yasiyotumia funguo na kuyakuta salama isipokuwa magari matatu tu ndio yalikuwa na mashaka ya kiusalama.

Matoleo mapya ya magari ya Discovery na Range Rover, na toleo la mwaka 2018 la Jaguar i-Pace, ambayo yote yanatengenezwa na kampuni ya Jaguar Land Rover yamekutwa salama.

Biashara
Maoni