Wachimbaji wadogo wa dhahabu waonywa

|
Uchimbaji holela wa madini ya dhahabu

Serikali imewataka wachimbaji wadogo wa Madini nchini kufanya shughuli zao katika maeneo yaliyopimwa lengo likiwa ni kupata uhakika wa uchimbwaji wa dhahabu katika maeneo yanayotambulika ili kuepuka uchimbwaji wa mashimo mengi yasiyo na tija.

Naibu Waziri wa Madini, DOTTO BITEKO ameyasema hayo katika Kijiji cha Byatika, Kata ya Buhemba wilayani Butiama mkoani Mara wakati akifungua mafunzo ya wachimbaji wadogo yatakayowasaidia kuongeza uzalishaji katika uchimbaji wao.

Ameyasema hayo baada ya Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Jiolojia na utafiti wa Madini Tanzania kueleza kupatikana kwa tani nyingi katika moja ya eneo ambalo lilitumika kama sampuli ambapo uchimbaji unaweza kufanyika kwa miaka 24.

Madini
Maoni