Wafanyabiashara Tanzania na Uganda watangaziwa neema

|
Waziri wa Usafirishaji wa serikali ya Uganda, Monica Mazubantege

Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Uganda na Tanzania wametakiwa kujiandaa kutumia  fursa ya  usafiri nafuu wa reli na maji kati ya nchi hizo hususan ziwa Victoria  ili kukuza biashara na uchumi kwa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki.

Hayo yamesemwa jijini Mwanza na Waziri wa Usafirishaji wa serikali ya Uganda, Monica Mazubantege kwenye ziara yake iliyolenga kukagua maendeleo ya uimarishaji wa Bandari ya Mwanza ambapo amesema kukamilika kwa ujenzi wa reli ya Standard Gauge na Bandari ya Bukasa, Uganda kutasaidia kupunguza gharama  kwa wasafirishaji wa bidhaa na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania na Uganda.

Ziara hiyo ya ujumbe kutoka Uganda ilianzia Dar es Salaam  na kujionea miradi mbalimbali ya sekta ya uchukuzi inayotarajiwa kuleta tija kwa Tanzania na Uganda ikiwemo upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam na ujenzi wa reli ya kisasa

Biashara
Maoni