Walizi wa mali za baharini washutumiwa kwa rushwa

|
Baadhi ya wavuvi wa Lindi na Mtwara wanaolalamikia BMU kukiuka makubaliano

Baadhi ya viongozi wa vikundi shirikishi vya ulinzi wa mali za bahari (BMU) wamelalamikiwa kujihusisha na vitendo vya kutoka kwa baadhi ya wavuvi ambao wamekiuka makubaliano ya kupumzisha mwamba wa bahari kwa kila baada ya miezi mitatu.

Kutokana na tuhuma hizo za rushwa inadaiwa baadhi ya wavuvi bado wanavua Pweza kinyume na utaratibu waliojiwekea.

Uvuvi ni moja ya shughuli  kuu  inayotoa ajira kubwa kwa wakazi wengi wa mikoa ya Lindi na Mtwara hususan kwa wale wanaishi kando ya Bahari ya Hindi na Mto Ruvuma.

Wenyeji  hao wanasema  ya kuwa kutokana na ukiukwaji wa makubaliano hayo, upungufu wa samaki na pweza umeanza kuonekana.

Katibu wa  doria  wa Somanga Kaskazini, Bashiru Bakari akijibu tuhuma hizo amesema, tatizo hilo halisababishwi na vikundi vya BMU isipokuwa baadhi ya wavuvi wenyewe kushindwa kuwa na msimamo hali inayosbabisha vikundi hivyo kuingia lawamani.

Hamisi Mussa Juma ni Mratibu wa Usimamizi wa Shirikishi la Uvuvi kutoka Shirika la Kimataifa la Uhifadhi Mazingira (WWF) anasema upatikanaji wa pweza kwa wingi umetajwa kuwa ni matokeo ya Wanavikundi vya Ulinzi wa Rasimali za Bahari (BMU) katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo kwa kiasi kikubwa wamesimamia elimu ya ulinzi shirikishi wa rasimali za bahari.

Kwa mujibu wa msimamizi huyo, iIwapo wananchi wa maeneo ya fukwe za bahari wataiga mfano huo wa Ulinzi wa Rasimali za Bahari kwa kutumia vikundi vya BMU wataweza kuongeza upatikanaji wa samaki nchini.

Utawala
Maoni