Xi Jinxing aahidi kufungua fursa zaidi za kimataifa

|
Mkutano wa Biashara za Kimataifa unaoendelea huko Shanghai, China

Rais wa China, Xi Jinxing amesema nchi yake imedhamiria  kuifungulia dunia milango ya kibiashara zaidi na zaidi huku akitumia mkutano wa kimataifa wa kibiashara kuitangaza China kama muagiza na muuzaji wa bidhaa.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Biashara za Kimataifa huko Shanghai, China, Rais Xi hakujibu  lolote juu ya misimamo ya Marekani na nchi za Ulaya dhidi ya Sera za Teknolojia na vikwazo kwa biashara ya kigeni.

Itakumbukwa hivi karibuni Marekani ilitangaza kupandisha asilimia 25 ya ushuru kwa bidhaa za China zilizo na thamani ya dola bilioni 34, miongoni mwao zikiwa bidhaa za elektroniki, teknolojia ya juu na vifaa vya kompyuta vya kuhifadhia data.

Katika hotuba yake Xi ameweka kando mgogoro huo na kutetea "ushirikiano kwa wote na utangamano, katika mkutano huo unaohudhuriwa na kampuni takribani 3,600 na viongozi wa kigeni akiwemo Waziri Mkuu wa Urusi, Dmitry Medvedev na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata.

“ China itabaki kuwa mtetezi mwenye nguvu wa uwazi katika ngazi ya kimataifa na itaendelea kuwa injini imara ya ukuaji wa uchumi wa kimataifa, soko kubwa na muhimu na fursa kubwa na mshiriki wa mageuzi ya kimataifa” alisema Xi.

Hata hivyo Rais Xi alikiri kwamba baadhi ya viwanda viko katika hatari ya kuporomoka lakini jitihada za kuvinusuri zimeshachukuliwa.

Biashara
Maoni