Beckam na Victoria kunadi nguo zao za harusi

|
David Beckam na mkewe Victoria wakati wa harusi yao mwaka 1999 (kulia) na walivyoonekana siku ya harusi ya Harry na Meghan (kushoto)

Walibeba vichwa vya habari wakati walipohudhuria harusi ya Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan Markle mwezi uliopita.

Na hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Instagram, jana Alhamisi ameweka wazi yeye na mkewe  Victoria wanapiga mnada nguo zao walizovaa.

Akiwa ameshika tangazo linalosomeka 'tuunge mkono katika wazo hili zuri la nguo zetu za harusi kuwa na matokeo bora', mcheza soka nyota wa zamani wa kulipwa mwenye miaka 43, David Beckam, katika kichwa cha habari cha picha hiyo amesisitiza kuwa fedha itakayopatikana itakwenda kwa familia zote zilizoathiriwa na shambulio la kigaidi la mwaka jana lililotokea jijini Manchester.

Beckam na Victoria wanatarajia kupiga mnada nguo zao za harusi walizovaa wakati wa harusi ya mwaka 1999 ikiwa imepita miaka 19

Maisha
Maoni