Beyonce atoa ofa kwa shabiki anayekula mbogamboga

|
Beyonce (kulia) akiwa ameambatana na mumewe Jaz Z, ambaye kwa sasa inadaiwa anakula vyakula vya mbogamboga tu

Mwanamuziki Beyonce ametoa ofa kwa mashabiki wake  wa Marekani kwaajili ya kujishindia tiketi ya bure kushuhudia shoo yake ya “for Life” akishirikiana na mumewe Jay Z.

Katika Ofa hiyo mwanamama huyo maarufu ametoa sharti kwa mshindi kuhakikisha anajitoa kwa dhati kula zaidi vyakula aina ya mbogamboga almaarufu “vegan meals”.

Hata hivyo ofa hiyo ambayo  Beyonce ameitoa kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye idadi ya wafuasi  milioni 123 ni ya mtu mmoja tu ambaye pia anatakiwa asizidi miaka 30.

Beyonce anaendesha shindano hilo kupitia mradi wake wa Greenprint ambao unaelezea faida chanya za ulaji wa vyakula vya mbogamboga ambazo pia zinahusika katika utunzaji wa mazingira.

Shindano hilo linawataka mashabiki hao kutuma aina ya vyakula vya kupandwa bustanini na mshindi atajipatia nafasi ya kushinda tiketi itakayodumu kwa miaka 30.

Chakula
Maoni