Beyonce awaleta wenzake wa Destiny Child pamoja

|
Kundi la Destiny Child lilipokutana kwa mara nyingine jijini Califonia kwenye Tamasha lililoandaliwa na Beyonce

Mwanamuziki Beyonce amefanikiwa kuwaleta pamoja wanamuziki wenzake wa kundi lao enzi hizo, Kelly Rowland na Michelle Williams wakati wa tamasha la jijini California usiku wa mwishoni mwa wiki.

Washiriki hao watatu wa Destiny Child walianza kutumbuiza kwa kushtukiza kwenye tamasha hilo kwa kushambulia jukwaa hilo kwa wimbo wao uliovuma mwaka 2004 wa Lose My Breath, ukafuatiwa na ule wa Say My Name na kumalizia na Soldier.

Hii ni mara yao ya kwanza kutumbuiza pamoja tangu mwaka 2015 waliposhiriki kwenye Tuzo za Muziki wa Injili  za Stellar.

Onesho hilo la mwanamuziki huyo mwenye miaka 36 lilianza kwa maudhui ya kijeshi ambapo ulipigwa kwanza wimbo wake uliovuma sana mwaka 2003 wa Crazy In Love ulipigwa na bendi ya watembea kwa miguu.

Wachezaji wake walivalia surualia nyeusi na masweta ya njano yaliyowekewa nakshi kama mavazi ya jeshi.

Kundi la Destiny Child ni miongoni mwa makundi yaliyofanikiwa zaidi kwa upande wa wanawake wakati wote nchini Uingereza.

Wanawake hao walishambulia jukwaa kwa kucheza kwa nguvu zote wakitumia kila kiungo kunogesha onesho hilo sanjari na kupiga saluti na kuchangamana na umati wa mashabiki waliofurika kwenye tamasha hilo.

Muziki
Maoni