Beyonce na Jay Z kutikisa pamoja ziara ya muziki Ulaya

|
Mwanamuziki Jay Z na mkewe Beyonce wanaotarajiwa kuanza ziara ya muziki pamoja

Mwanamuziki Beyonce na Jay-Z wamethibitisha kuwa pamoja katika ziara ya onesho litakalojulikana kama ‘On The Run II, ‘.

Uthibitisho huo umetangazwa kupitia tangazo la video la wawili hao wakiwa pamoja ambalo pia Beyonce amelituma kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mashabiki wao walioanza kubashiriki ushiriki wa pamoja katika ziara hiyo ya muziki baada ya kuona orodha kadhaa za matangazo ya tiketi pamoja na kusheheni kwa matangazo hayo kwenye ukurasa wa Facebook wa Beyonce.

Katika ziara hiyo ya muziki, Uingereza wamepangiwa siku nne katika mwezi Juni.

Maisha
Maoni