Brad Pitt amjibu Jolie madai ya kutotunza watoto

|
Brat Pitt wakati huo akiwa na familia yake ambayo sasa yeye na mtalaka wake wameingia kwenye vita ya matunzo ya watoto

Mwigizaji wa Filamu nyota wa Marekani, Brad Pitt amejibu madai yaliyowasilishwa na mtalaka wake, Angelina Jolie kuwa ameshindwa kusaidia watoto wao.

Katika kesi iliyofunguliwa jana, Jumatano, timu ya sheria ya nyota huyo imesema mpaka sasa ameshalipa zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 1.3 kwaajili ya gharama za matumizi mbalimbali sanjari na mkopo wa dola milioni 8 za Marekani aliompa Jolie kumsaidia kununua nyumba.

Jumanne juma hii, wakili wa Jolie alisema Pitt hajawahi kulipa "mchango wowote wa maana kwaajili ya kusaidia malezi ya watoto" tangu talaka itolewe mwaka 2016.

Wawili hao walikaa pamoja kama wapenzi tangu  2005 na baadaye mwaka 2014 walifunga ndoa iliyodumu kwa miaka miwili.

Katika nyaraka zake, wakili wa Pitt amesema, madai ya Jolie kuhusu matunzo ya watoto ni " jitihada dhaifu kwaajili ya kuvilaghai vyombo vya habari vimpatie fursa."

Hakuna majibu ya haraka mpaka sasa kutoka kwa wawakilishi wa Jolie.

Maisha
Maoni