Buriani mbunifu wa mitindo maarufu duniani

|
Hubert de Givenchy, wakati wa uhai wake katika moja ya maonesho yake ya mitindo

Mbunifu wa mitindo maarufu duniani na raia wa Ufaransa, Hubert de Givenchy, ambaye aliunda mtazamo wake maarufu kupitia mwanamtindo Audrey Hepburn na Jackie Kennedy, amefariki dunia akiwa na miaka 91.

Mshirika mwenza Philippe Venet, mbunifu maarufu wa mitindo mbalimbali ameithibitishia AFP kufariki kwa mbunifu huyo mwenye jina kubwa.

"Ni masikitiko makubwa, tunapenda kuwafahamisha kuwa Hubert Taffin de Givenchy amefariki dunia," alisema kupitia taarifa yake.

Katika taarifa hiyo ndugu wa kike na wa kiume pamoja na watoto wa mbunifu huyo walishiriki katika kuelezea masikitiko yao.

Givenchy huenda ndiye mbunifu maarufu zaidi duniani kupitia mtindo wake maarufu wa gauni jeusi fupi alilowahi kuvaa mwanamitindo Audrey Hepburn kwenye ufunguzi wa tukio la kifungua kinywa katika mgahawa maarufu wa Tiffany.

Maisha
Maoni