Diamond Platnumz na Rayvanny waiangukia BASATA

|
Diamond Platnumz na Rayvanny wameonesha video fupi ya dakika moja wakiomba radhi kwa watanzania na wizara inayohusika na sanaa sambamba na BASATA.

Msanii nyota wa Pop, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mwenake Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ wameomba radhi kwa Baraza la Sanaa nchini (BASATA).

Wawili hao wakionekana kwenye video waliyojirekodi huku Diamond akiwa ndiye mzungumzaji wamesema wamefanya makosa na wanaomba radhi.

Japo tunajitahidi kuwa vijana wa mfano bora kwenye Taifa letu, lakini kama tulivyoumbwa binadam hatuwezi kupatia siku zote, lazma itatokea siku tutateleza tu....”

“Ila Utelezapo, ni vyema kulijua Kosa na Kulirekebisha ili kesho na Kesho kutwa lisijirudie....”

“Inshaallah Mwenyez Mungu Atusimamie na kutuongezea Juhudi na Maarifa katika Kazi zetu ili kwa Pamoja tuzidi kuukuza Muziki wetu na Kuendelea Kuiwakilisha vyema na kulipa sifa Nzuri na Heshima Nchi yetu....Tuseme Amin.....

Wawili hao walifungiwa kufanya maonesho nje na ndani ya Tanzania kwa muda usiojulikana kufatia kukaidi amri ya BASATA ya kutoutumia wimbo wao wa Mwanza ambao pia waliamriwa wauondoe mtandaoni.

Katika maonesho ya kundi la Wasafi linaloongozwa na Diamond Platnumz yaliyokuwa yakifanyika kwenye mikoa mbalimbali wimbo Mwanza ulikuwa ukitumika.

Maisha
Maoni