Fid Q auaga ukapera, wengi wampongeza

|
Mwanamuziki Fareed Kubanda aka Fid Q akiwa katika picha mkewe baada ya kufunga ndoa Januari Mosi

Msanii wa Hip hop nchini, Fareed Kubanda maarufu Fid Q ameuanza mwaka 2019 kwa kufanya uamuzi muhimu wa kufunga ndoa na aliyekuwa mpenzi wake wa siku nyingi aliyejulikana kwa jina la ‘Mama Cheusi’

Ndoa hiyo ilifungwa Januari Mosi mwaka huu, katika Msikiti wa Qiblatain Boko Jijini Dar es Salaam baada ya kumvisha pete mwanamke huyo mwishoni mwa mwaka jana, Disemba 31.

Katika sherehe ya harusi yao mastaa mbalimbali walishiriki kwa ajili ya kumpongeza msanii mwenzao aliyeamua kuuaga ukapela akiwemo Ambwene Yessaya (AY) ambaye pia ametupia baadhi ya picha za tukio hilo katika ukurasa wake wa Instagram.

“Hongera sana ndugu yangu kwa kufunga ndoa, Mwenyezi Mungu aibariki ndoa yenu, ” aliandika AY.

Baada ya matukio hayo mashabiki na wasanii wenzake wengine wamemtuma salama za pongezi pamoja na kumtakia kheri katika ndoa yao hiyo.

Maisha
Maoni