Forbes yamtaja Kylie Jenner kuwa ndiye bilionea mdogo zaidi

|
Bilionea Kylie Jenner akiwa katika ofisi yake inayojishughulisha na masuala ya vipodozi

Habari za mkanganyiko wa mambo hazijawahi kuiacha mbali familia ya Kardashian.

Lakini safari hii, siyo kuhusu suala la watoto au wapenzi wao wa kiume waliobeba vichwa vya habari bali ni mmoja wa binti wa Kris, Kylie Jenner ambaye ametambulishwa kama mmoja wa matajiri vijana anayekadiriwa kutengeneza mabilioni ya dola.

Jenner, ambaye  aliyetambulishwa na Jarida la Forbes akishika nafasi ya 10 ya utajiri akiwa na miaka 21,  anatambulika kimataifa zaidi kupitia Kipindi chao cha maisha halisi ya familia yao kinachojulikana kama Keeping Up with the Kardashians.

Licha ya Jenner kutangazwa kwamba utajiri wake huo umetokana na kufanya vema katika mauzo ya biashara zake za vipodozi, maarufu kama  Kylie Cosmetics, baadhi ya watu wamehoji iwapo fedha hizo ni kweli zimetokana na ‘jitihada zake binafsi’ ,

Jenner ameikaribisha hadhi hiyo ya ubilionea kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuishukuru Forbes kwa kumtambua.

Aidha ametetea dhana ya kuwa bilionea kwa jitihada zake binafsi akisema katika fedha yote hiyo hakuna fedha ya urithi na kusema kuwa "Ni kweli utajiri huo ni jitihada zake".

Amedai kuwa alipokuwa na umri wa miaka 15, wazazi wake, Kris na Caitlyn Jenner, walimuondoa katika kuwategemea na kumweleza kuanza kujitafutia utajiri wake mwenyewe.

Kwa upande wa Forbes wameelezea namna wanavyopima suala hilo kwa kusema: "Ili kuweka hili wazi, Forbes tunaitafsiri "jitihada binafsi" kama mtu ambaye ameijenga kampuni na kuwezesha kujipatia utajiri wake mwenyewe, badala ya kurithishwa kiasi au wote."

Maisha
Maoni