Harry na Meghan washiriki maadhimisho ya kuzaliwa malkia pamoja

|
Harry na Meghana wakiwa miongoni mwa wanafamilia waliojumuika kwenye maadhimisho ya miaka 93 ya Malkia Elizabeth

Mke wa mtawala wa Sussex ameonekana kwa mara ya kwanza kwenye kibaraza cha kasri la Buckingham leo, Jumapili, akiwa ameambatana na mumewe Harry,  Watawala wa Cambridge, wakiwa ni miongoni mwa wanafamilia waliohudhuria sherehe ya kuadhimishi miaka 92 ya kuzaliwa kwa Malkia Elizabeth.

Kukiwa na uvumi wa wawili hao kuwa katika mapumziko yao mafupi nchini Ireland katika mji wa Co. Mayo, wana ndoa hao wapya walionekana wenye furaha na utulivu wakati wa kutoa heshima zao kwa Malkia katika sherehe zilizofana na kupambwa na kikosi cha farasi weupe.

Malkia huyo alionekana mwenye tabasamu pana mara baada ya kumuona mwanaye mwana Prince Charles, Andrew na William, pamoja na Princess Anne wakiwasili kwa gari la farasi katika sherehe hizo huku akiwa amevua miwani baada ya kufanyiwa upasuaji wa macho wiki tatu zilizopita.

Makumi kwa maelfu ya wapenzi wa familia ya kifalme waliokusanyika kwenye barabara za eneo ambalo gwaride hilo lilifanyika huku wakionesha furaha na shauku ya kuiona familia nzima ya kifalme ikiwa pamoja katika kibaraza cha kasri la malkia huku Meghan na Kate wakibadilishana mawazo huku Harry akiangalia matukio hayo kwa umakini. 

Katika sherehe hizo Meghan alivaa gauni lilibuniwa na Carolina Herrera na kofia iliyobuniwa na Philip Treacy. Wakati Kate alivalia Alexander McQueen na kofia kutoka kwa mbunifu Juliette Botterill.

Camilla yeye alivalia gauni la silki rangi ya bluu na koti lililobuniwa na Bruce Oldfield na kofia ya Philip Treacy huku malkia akivalia koti la bluu lilibuniwa na Stuart Parvin, na kofia ikibuniwa na Angela Kelly

Maisha
Maoni