Harusi ya Harry na Meghan kuwa ya kitofauti

|
Miongoni mwa watoto wa rafiki wa karibu wa bibi harusi Meghan wanaotarajiwa kusimamia harusi hii

Maandalizi ya harusi ya Kifalme ya Prince Harry na Meghan Markle imeendelea kuleta msisimko wa kipekee baada ya wawili hao kuvunja mwiko wa harusi za kifalme katika suala la wasimamizi wao.

Katika harusi hiyo, inadaiwa kuwa wasimamizi wa kike na wale wa kiume wengi wao wanatarajiwa kuwa watoto wa marafiki wa karibu wa Prince Harry na Meghan Markle.

Inadaiwa kuwa katika harusi hiyo inayotarajiwa kufanyika kwenye kasri la Windsor itakuwa na hisia isiyozoeleka baada ya wawili hao kuangalia nje ya familia ya kifalme kwa kuruhusu wavulana na wasicahan kumi kusimamia harusi hiyo.

Kati ya hao ni watoto wawili tu ndiyo watakaokuwa wakitoka katika familia ya kifalme ambao ni watoto wa kaka yake Bwana harusi, Princess Charlotte mwenye miaka mitatu na Prince George mwenye miaka minne.

Watoto watatu watakuwa ni wa rafiki yake wa karibu bibi harusi Jessica Mulroney ambao ni mapacha wake Brian na John, wenye miaka saba, na binti yake Ivy mwenye miaka minne siku hiyo ya Jumamosi.

Baba ya watoto hao ni Ben Mulroney, ambaye ni mtoto wa kiume wa aliyewahi kuwa Waziri mkuu wa Canada, Brian Mulroney.

Warembo watoto watakaosindikiza harusi hiyo katika kanisa la St George kwenye viwanja vya kasri hilo ni pamoja na watoto wa ubatizo wa Harry, Zalie Warren mwenye miaka miwili na Florence van Cutsem mwenye miaka mitatu.

Maisha
Maoni