Hospitali yaruhusu ndoa kufungwa wodini baada ya bwana harusi kulazwa

|
Harusi baina ya Hercules na Maryam ililazimika kufungwa kwenye wodi ya hospitali ya Gatesville Melomed baada ya mwanaume kulazwa kufuatia kushambuliwa na majambazi kwenye tukio lililotokea siku moja kabla ya siku ya ndoa.

Uongozi wa hospitali ya Gatesville Melomed nchini Afrika Kusini ililazimika kuruhusu kufanyika kwa sherehe kwenye moja ya wodi zake baada ya mmoja wagonjwa wake kulazimika kufunga ndoa hospitalini hapo.

Bwana harusi, Muneer Hercules alishambuliwa kwenye tukio la uporaji na kulazimika kulazwa kwenye hospitali hiyo siku moja kabla ya siku ya ndoa.

Kwakuwa harusi ilikuwa imeshapangwa ikalazimu hospitali hiyo “kutoa msaada wa kipekee” kwa kuruhusu dnoa kufungwa wakati bwana hrusi akiwa kitandani na sherehe ndogo kufanyika hospitalini hapo ikiwahusisha ndugu wachache wa familia.

Hercules alimuoa mchumba wake Marya Kallile siku ya Jumapili baada ya kushambuliwa usiku wa siku ya Jumamosi.

Maisha
Maoni