Jay-Z na Beyonce wadaiwa kurudia viapo vya ndoa yao

|
Picha zilizoonesha wawili hao kurudia viapo vya ndoa pamoja na watoto wao mapacha Rumi na Sir

Wakiwa katika ufunguzi wa onesha lao la ziara ya kimuziki inayojulikana kama ‘On The Run II tour’ katikati ya juma usiku, wanandoa Jay Z na mkewe Beyonce walionesha sehemu ndogo ya sherehe yao ya hivi karibuni wakati wakirudia viapo vya ndoa katika kutimiza miaka 10 iliyoadhimishwa mwezi Aprili.

Vipande vya video hiyo ilirusha katika onesho hilo, sehemu ambayo wawili hao walivalia nguo za harusi ambazo siyo walizozivaa mwaka 2008 wakati wakifunga ndoa yao ya kifahari mwaka huo.

Katika ufunguzi huo wa onesho la kuanza kwa ziara hiyo ya kimuziki, wapenzi hao wawili wenye nguvu walianza kwa kuonesha shoo ya nguvu wakisindikizwa na vipande vya video zilizoonesha sehemu za nyumba yao katika mpangilio mzima wa kimahaba sanjari na watoto wao mapacha wenye mwaka mmoja Rumi na Sir pamoja na dada yao mwenye miaka sita Blue Ivy. 

Maudhui ya ziara yao hiyo yanafuatiwa na lile la awali walilofanya pamoja mwaka 2014 ililofahamika kwa 'This Is Real Love', ikithibitisha kuwa ndoa yao sasa iko kwenye mwamba imara.

Uhusiano wa wawili hao awali ulipita kwenye mawimbi mazito na kuhitimishwa na ziara yao ya muziki iliyoangaliwa na dunia yote ya wapenzi wa muziki. 

Kuyumba kwa uhusiano huo kulianza mwaka 2014 wakati wa Met Gala kulipotokea sintofahamu na vipande vya video kuvuja vikionesha mdogo wake Beyonce, Solange na Jay Z wakishambuliana katika lifti.

Pia mwaka 2016 mwanamuziki Beyonce alitoa albamu iliyojulikana kwa jina la Lemonade ikianika hisia zake zote juu ya kukosekana kwa uaminifu kwenye uhusiano wake na namna njia za uovu inavyoweza kumtenda vibaya mwanamke anayekupenda', na kumtambulisha mwanamke Becky mwenye nywele nzuri.

Wakati huo huo naye Jay-Z akitoa albamu ya 4:44  'ikiwa ni album ya kuomba msamaha' ikionesha kukubali kuwa na mapenzi na wanawake wengi na kuafiki kuwa imegharimu maisha ya familia yake.

Maisha
Maoni