John Cena atangaza kuachana na mpenzi wake Nikki

|
John Cena na Nikki enzi za mapenzi motomoto

Mcheza mieleka nyota, John Cena na mpenzi wake wa muda mrefu Nikki Bella wametangaza kuachana rasmi .

Wawili hao waliochumbiana kwa takribani miaka sita, wameandika taarifa ya pamoja jana, Jumapili wakisema: 'Wakati uamuzi huu ukiwa ni mgumu kwetu, tumeamua kuendelea kupendana na kuheshimiana kwa kila mmoja wetu. Tunawaomba muheshimu faragha yetu wakati huu tunaoendelea na maisha yetu.'

Uamuzi huo umefikiwa huku wawili hao walishapanga mwezi Ujao wa Mei 5, kuwa ndiyo siku yao ya ndoa.

Cena, mwenye miaka  40, aliweka taarifa hiyo kwente mitandao ya kijamii iliyoambatana na picha za mvunjiko wa moyo na kuweka maneno yaliyowahi kusemwa na Walt Whitman, yakisomeka: 'Tuko pamoja. Nasahau yaliyosalia.'

Jonh hivi karibuni ameigiza filamu iliyopewa jina la Blockers, ambapo amecheza kama baba anayejaribu kumshauri binti yake asikubali kupoteza bikira yake katika usiku wa sherehe za usiku zinazoandaliwa na shule.

Na kusema sehemu hiyo aliyoigiza ilisababisha mazungumza magumu na mpenzi wake Nikki, ambaye alitaka kuwa mama.                                                                                                              

Inasemekana wawili hao hivi karibuni wamekuwa kwenye mgogoro na vuta nikuvute kutokana na suala la kupata watoto huku John Cena ikidaiwa kuwa hayuko tayari kwa hilo.

Maisha
Maoni