Kashfa ya udhalilisha wa Kingono yamfikisha R.Kelly Polisi

|
Mwanamuziki nyota wa Marekani, R. Kelly akiwasili katika kituo cha Polisi mjini Chicago kufuati mashtaka yanayomkabili ya madai ya kudhalilisha wasichana kingono

Mwanamuziki Robert Kelly hatimaye amefunguliwa mashtakiwa 10 yanayo muhusisha na makosa ya unyanyasaji wa kijinsia uliosababishwa na uhalifu wa kingono huku makosa tisa kati ya hayo yakidaiwa kuhusisha watoto.

Mwanamuziki huyo nyota wa nyimbo za R&B, ambaye jina lake halisi ni  Robert Sylvester Kelly, amekuwa katika kashfa ya madai ya kudhalilisha kijinsia wanawake na wasichana wadogo kwa miongo kadhaa sasa.

Alishawahi kushtakiwa lakini alikanusha madai yote yaliyoelekezwa kwake kwa madai hayakuwa na ukweli wowote.

Nyaraka za kuamuru kukamatwa kwake zilitolewa mwishoni mwa Juma, siku ya Ijumaa ambapo mara baada ya kupata taarifa hiyo R. Kelly mwenye miaka 52 alijisalimisha mwenye Polisi jijini Chicago.  Mwanasheria wake amesema mwanamuziki huyo kwa sasa amekuwa "kwenye mashaka makubwa".

Steve Greenberg amelieleza Shirika la Habari la Associated Press kuwa mteja wake amekuwa  "mwenye mawazo na shinikizo kubwa" kutokana na mashtaka hayo na kusisitiza kuwa hana hatia.

Tukio hilo limekuja ikiwa zimepita juma kadhaa tangu kutolewa kwa Makala ya mfululizo iliyohusisha simulizi za waathirika wa matendo ya unyanyasaji wa kijinsia waliofanyiwa na nyota huyo iliyoitwa ‘Surviving R Kelly .

Maisha
Maoni