Kibatala amtosa Wema, Msando aokoa jahazi Mahakamani

|
Nyota wa Filamu nchini, Wema Sepetu akitoka mahakamani

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Januari 10, 2018 imeahirishwa kesi inayomkabili Malkia wa filamu Bongo, Wema Sepetu,  hadi Februari 8, mwaka huu.

Uamuzi huo umekuja kufuatia Mahakama hiyo kupokea barua mbili kutoka kwa Wakili wa Wema, Peter Kibatala ya kujitoa katika kesi hiyo ya Wema na kupokea barua nyingine kutoka kwa Wakili, Alberto Msando kuwa ndiye atakayemwakilisha sasa kama Wakili mpya.

Wema anakabiliwa na kesi ya kukutwa na misoko ya bangi nyumbani kwake.

Maisha
Maoni